King alifanya hivyo akizingatia kuwa mafanikio ya harakati hizo zingeweza kufanikiwa tu kwa kufuata misingi ya kuepukana na uvunjifu wa amani.
Kila mwaka Jumatatu ya tatu ya mwezi Januari, Wamarekani wanamuenzi kiongozi wa haki za raia aliyeuwawa ambaye katika miaka ya 1950 na 1960 aliandaa maandamano ya amani dhidi ya ubaguzi, ikiwa ni harakati za kutafuta haki za watu weusi na kuwawezesha kupiga kura.
Wengi nchini wanatumia siku ya mapumziko kumkumbuka King kwa kutokuchoka katika kukomesha ubaguzi kwa kushiriki katika shughuli za huduma za kijamii.
Bunge la Marekani lilimuenzi King kwa ule moyo wake wa kutumikia jamii mwaka 1994 kwa kuifanya siku hiyo ni mapumziko iwe ni siku ya kuhudumia taifa.
Rais Donald Trump amemuenzi King wakati wa sherehe za kuadhimisha kumbukumbu yake mjini Washington Ijumaa, akipongeza hatua yake ya “kupigania haki na usawa kwa amani.”