Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:40

Ni nani Martin Luther King Jr.?


Farasi akivuta jeneza la Dkt Martin Luther King Jr lililopitishwa katika mitaa ya Atlanta, April 10, 1968, likielekea katika nyumba ya kuhifadhia maiti Chuo cha Morehouse.
Farasi akivuta jeneza la Dkt Martin Luther King Jr lililopitishwa katika mitaa ya Atlanta, April 10, 1968, likielekea katika nyumba ya kuhifadhia maiti Chuo cha Morehouse.

Martin Luther King Jr., ni muasisi wa harakati za haki za kiraia nchini Marekani, ambaye aliuwawa zaidi ya miaka 50 iliyopita, Aprili 4, 1968.

Mwanzo wa maisha yake

Martin Luther King Jr. alizaliwa Jan 15, 1929, katika mji wa Atlanta, Jimbo la Georgia. Alikuwa ni mtoto wa Martin Luther King Sr., ambaye ni mhubiri maarufu na kiongozi wa kupigania haki za raia, na mama yake Alberta King, ambaye alikuwa ni mwalimu.

King anasema kuwa alikuja kuwa na ufahamu zaidi juu ya ubaguzi katika umri wa miaka 6, wakati baba wa moja wa rafiki zake ambaye ni mzungu alikuwa hawezi kumruhusu mtoto wake kucheza naye.

Maandalizi ya maandamano

King alipata umaarufu katikati ya kipindi cha mwaka 1950 wakati kama mhubiri kijana aliongoza kwa mafanikio harakati za kuondoa ubaguzi ulioigubika sekta ya usafiri wa mabasi ya umma huko mjini Montgomery, Jimbo la Alabama, akisukuma mji huo kuondoa vitendo vya ubaguzi kwa abiria ambao ni watu weusi.

Aliandaa maandamano kupinga ubaguzi huo kipindi chote cha mwaka 1950 na 1960 dhidi ya ubaguzi ulio kuwepo upande wa kusini ya Marekani kwa ajili ya kupigania usawa wa watu weusi na haki za kupiga kura.

Falsafa ya amani

King alikuwa anafahamu njia kuu ya mafanikio katika harakati za haki za kiraia ilikuwa ni kufuata mkakati wa kuandamana kupinga ubaguzi bila ya uvunjifu wa amani, ikiwa ni njia mbadala wa harakati za kutumia silaha.

King amesema alikuwa amehamasishwa na mafundisho ya kiongozi wa India Mahatma Gandhi.

Harakati hizo za kupinga ubaguzi zilijaribiwa katika maeneo kama vile Birmingham, Alabama, ambako polisi walitumia mbwa washambuliaji na maji ya zima moto kuwatawanya waandamanaji watoto wa shule na huko Selma, Alabama, ambako maandamano ya 1965 yanakumbukwa kama "Bloody Sunday" (Umwagaji wa damu siku ya Jumapili) kutokana na polisi kuwashambulia na kuwajeruhi waandamanaji.

Maandamano ya Mjini Washington

Hotuba ya King maarufu “I Have a Dream” (ninayo ndoto) ilianzisha kile kilichokuwa ni harakati za watu wengi zaidi weusi wa upande wa Kusini na kampeni hizo za kupigania haki za raia kuenea nchini kote Marekani.

Ilipofika August 1963, msukumo huo muhimu wa kuleta haki uliongozeka nchini kote, na watu weusi na wazungu 250,000, walisafiri kwenda makao makuu ya Marekani; kushiriki katika mandamano hayo yaliyofanyika Washington. Maandamano hayo yalifanyika kwa amani na hapajakuwa na kukamatwa kwa mtu yeyote.

Ushindi wa kisiasa

Harakati za haki za binadamu zilifikia kilele chake mwaka 1964, wakati Rais Lyndon Johnson aliposaini Sheria ya Haki za Raia ikipiga marufuku ubaguzi wa rangi katika maeneo ya umma na King alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel. Mwaka uliofuatia, Sheria ya Haki ya Kupiga Kura ilizuia vitendo vilivyo kuwa vikifanywa na wabaguzi kuwazuia watu weusi kushiriki kupiga kura.

Kuuwawa King

April 4, 1968, King aliuwawa kwa kupigwa risasi moja katika nyumba ya malazi mjini Memphis, Jimbo la Tennesse, ambako alikwenda kuwaunga mkono wafanyakazi wanao safisha mji walio kuwa katika mgomo. James Earl Ray, mbaguzi, ambaye alikiri kumpiga risasi King na kutumikia maisha yake yote Jela.

King, ambaye alikufa akiwa na miaka 39, alitoa hotuba usiku mmoja kabla ya kifo chake ambacho kiliashiria kuuwawa kwake. "Na tayari nimeiona ardhi iliyo ahidiwa, pengine sito weza kufika pale na nyinyi, lakini nataka mjue usiku huu kwamba sisi kama watu tutafika pale tulipoahidiwa," alieleza.

XS
SM
MD
LG