Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:59

Msimu wa sikukuu unaanza ukiwa na changamoto zilizoletwa na janga la COVID-19


Magari yakienda pole pole eneo la Pena Boulevard wakati msongamano ukiongezeka barabarani kuelekea sikukuu ya Thanksgiving Jumanne, Nov. 23, 2021, karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Denver.(AP Photo/David Zalubowski)
Magari yakienda pole pole eneo la Pena Boulevard wakati msongamano ukiongezeka barabarani kuelekea sikukuu ya Thanksgiving Jumanne, Nov. 23, 2021, karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Denver.(AP Photo/David Zalubowski)

Msimu wa sikukuu ambao unaanza na inaonekana utakuwa ni wa gharama kubwa zaidi kutokana na changamoto ambazo zimeletwa na janga ambalo limeathiri pia usambazaji chakula nchini Marekani.

Sikukuu ya Thanksgiving kiasili ni kwa wakulima na wazalishaji ambapo hutumia miezi kadhaa kupanga, na inatabiriwa mwaka huu haitakuwa ya kawaida kwa Wamarekani kwa vile itaumiza mifuko yao.

Sikukuu ya Novemba 25 ambayo inasheherekewa kila Alhamisi ya nne ya mwezi Novemba. Ilianzia mwaka 1621, pale wakoloni wa huko Plymouth na Wampanoag waliposhirikiana mavuno makubwa ya msimu wa vuli ambapo wanakiri hivi leo kuwa ni moja ya sherehe za kwanza kabisa za Thanksgiving katika makoloni hayo.

Kwa zaidi ya karne mbili sikukuu ya kumshukuru Mungu ilisheherekewa na maeneo binafsi na majimbo. Ilikuwa ni mpaka mwaka 1863, katikati ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambapo Rais wa Marekani wakati huo Abraham Lincoln alipotangaza siku ya Thanksgiving ni ya kitaifa na itasheherekewa kila mwezi Novemba.

Rais wa zamani Abraham Lincoln (image courtesy of the National Archives)
Rais wa zamani Abraham Lincoln (image courtesy of the National Archives)

Septemba mwaka 1620, meli ndogo iliyoitwa Mayflower iliondoka Plymouth, Uingereza, ikiwa imebeba abiria 102 – watu wa dini mbali mbali wakitafuta makazi mapya ambako wanaweza kwa uhuru kuabudu imani zao. Na watu wengine binafsi walivutiwa na ahadi ya ustawi na umiliki ardhi katika “Dunia Mpya.”

Baada ya safari yenye misukosuko na isiyokuwa rahisi ambayo ilidumu siku 66, walitia nanga karibu na Cape Cod, upande wa kaskazini mbali na azma ya sehemu ya kusimama kwenye mto Hudson. Mwezi mmoja baadaye, Mayflower ilivuka Massachusetts Bay, ambako mahujaji, kama wanavyojulikana hivi sasa, walianza kazi ya kuanzisha Kijiji huko Plymouth.

Novemba mwaka 1621, baada ya mavuno ya kwanza ya mahindi ya wahamiaji hao kuwa na mafanikio makubwa, Gavana William Bradford aliandaa sherehe za chakula na kuwakaribisha kundi la washirika wao wazawa wa Marekani, akiwemo chifu Massasoit wa Wampanoag.

Hivi sasa, inakumbukwa kama “Thanksgiving ya kwanza”, ingawaje mahujaji wenyewe huenda wasingetumia neno hilo wakati huo – sherehe hizo zilidumu kwa siku tatu.

Wakati hakuna rekodi iliyopo kuhusu mlo haswa wa Thanksgiving ya kwanza. Wanahistoria wamependekeza kwamba vyakula vingi huenda vilitayarishwa kwa kutumia viungo vya asili vya Marekani na mbinu zile zile za upishi.

Kwa sababu mahujaji hawakuwa na matanuri na usambazaji sukari ya Mayflower ulishuka yalipoingia majira ya fall mwaka 1621, mlo haukuwa na mikate mitamu, keki au vitinda mlo (dessert) ambavyo vimekuwa ni alama mahsusi kwa sherehe za sasa.

Katika nyumba za Wamarekani wengi, sherehe za Thanksgiving zimepoteza umuhimu wake wa asili; badala yake hivi sasa zimejikita zaidi katika kupika na kushirikiana mlo mkubwa pamoja na familia na marafiki. Bata mzinga, chakula kikuu cha Thanksgiving kila mahali na kinahusishwa na sikukuu, pengine kilikuwepo au la katika sherehe za kwanza za mahujaji mwaka 1621.

Leo, hata hivyo, takriban asilimia 90 ya Wamarekani wanakula bata, iwe ameokwa, amechomwa au kukaangwa, kwenye siku ya Thanksgiving, kwa mujibu wa National Turkey Federation. Vyakula vingine vya kiasili ni pamoja na stuffing, viazi vya kuponda, sausi ya cranberry na pai ya boga. Kujitolea ni moja ya shughuli maarufu sana siku ya Thanksgiving, na jamii mara nyingi zinakuwa na shughuli ya kugawa chakula cha bure kwa wale ambao wana shida.

Rais wa Marekani, Joe Biden aliungana na mke wake Dr. Jill Biden na Makamu Rais Kamala Harris na mume wake Dough Emhoff kwenye eneo maarufu la D.C Central Kitchen, wakisaidia kuwapatia chakula cha Thanksgiving wale ambao wana shida.

Rais Joe Biden, Mkewe Jill Biden, Makamu wa Rais Kamala Harris, na mumewe Doug Emhoff, wakitayarisha mifuko ya chakula cha Thanksgiving wakati walipotembelea Jiko la DC Central, Washington, Jumanne, Nov. 23, 2021.
Rais Joe Biden, Mkewe Jill Biden, Makamu wa Rais Kamala Harris, na mumewe Doug Emhoff, wakitayarisha mifuko ya chakula cha Thanksgiving wakati walipotembelea Jiko la DC Central, Washington, Jumanne, Nov. 23, 2021.

Biden, alifuatana na dazeni ya wana familia, na kwenda kwenye mapumziko ya sikukuu katika kisiwa cha Nantucket, kusheherekea fursa ya kwanza na kuepuka wiki kadhaa za habari mbaya.

Mfumuko wa bei uko juu baada ya takriban miongo mitatu, huku bei ya bata mzinga chakula cha Thanksgiving na vitafunio vingine inakadiriwa na shirikisho la American Farm Bureau kuwa imepanda kwa asilimia 14 kutoka mwaka 2020.

Ndege na viwanja vya ndege kote chini Marekani ni sehemu ambazo zinatarajiwa kuwa na harakati nyingi sana kwa vile wakati mamilioni ya Wamarekani wakisafiri kutembelea familia zao kwa ajili ya sikukuu ya Thanksgiving.

Mamlaka ya Usalama wa Usafiri (TSA) inatarajia kuwakagua abiria milioni 20 watakaotumia usafiri wa anga wakati wa sikukuu ya Thanksgiving, ikiwa ni idadi kubwa tangu mwaka 2019 wakati ambapo takriban Wamarekani milioni 26 walisafiri wakati huo, huku viwango vya watu kupatiwa chanjo ya COVID-19 vikiongezeka na kuwafanya watu kuwa na imani kubwa ya kufanya safari.

Shirika binafsi la usafiri kama AAA linakadiria, kwa jumla, watu milioni 53.4 watasafiri kwa ajili ya sikukuu ya Thanksgiving, ikiwa juu ya kutoka asilimia 13 mwaka 2020, huku usafiri wa anga ukirejea tena kwa kiasi cha asilimia 91 ya viwango vya kabla ya janga.

XS
SM
MD
LG