Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:29

Marekani na Russia zinajadili uwezekano wa kubadilishana wafungwa zaidi -Kremlin


Rais wa Russia Vladmir Putin 9Kushoto) na mwenzake wa Marekani Joe Biden
Rais wa Russia Vladmir Putin 9Kushoto) na mwenzake wa Marekani Joe Biden

Marekani na Russia zinajadili uwezekano wa kubadilishana wafungwa ambao unaweza kumhusisha mwandishi wa gazeti la Wall Street Journal, Evan Gersh-kovich, ambaye anazuiliwa katika gereza la Moscow, kwa tuhuma za ujasusi ambazo anakanusha.

Mfungwa wa pili ni raia wa Russia anayezuiliwa Marekani kwa tuhuma za uhalifu wa mtandaoni, Kremlin ilisema Jumanne.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari kwamba maafisa wa Russia na Marekani, wamejadiliana kuhusu kubadilishana wafungwa, hatua ambayo inaweza kuwahusisha Gersh-kovich, na Vladimir Dunaev, ambaye alihamishwa kutoka Korea Kusini, na yuko kizuizini katika jimbo la Ohio, nchini Marekani.

Siku ya Jumatatu, Marekani ilitoa idhini kwa Dunaev kuwasiliana na ubalozi wa Russia, kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake mwaka wa 2021, wakati Lynne Tracy, balozi wa Marekani mjini Moscow, alipotembelea Gersh-kovich, kwa mara ya pili tangu kukamatwa kwake, mwishoni mwa mwezi Machi.

Hakukuwa na dalili kwamba ubadilishanaji wa wafungwa hao ulikuwa karibu kufanyika, huku mahakama ya Russia ikitoa uamuzi wiki iliyopita kwamba Gersh-kovich anaweza kuwekwa kizuizini hadi Agosti 30, na nchi hiyo, mara nyingi ikisema kwamba ubadilishanaji wowote, haungeweza kufanywa hadi uamuzi wa kesi hiyo, utolewe.

Tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, bado haijatangazwa.

Forum

XS
SM
MD
LG