Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:08

Msaada wa magharibi kwa Ukraine dhidi ya Russia unaleta mabadiliko;Stoltenberg


Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg akizungumza na wanahabari wakati alipokuwa Oslo, Norway. June 1, 2023.
Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg akizungumza na wanahabari wakati alipokuwa Oslo, Norway. June 1, 2023.

Mashambulizi yameanzishwa na Wa-ukraine wanapiga hatua, na kusonga mbele, Stoltenberg alisema wakati alipokutana na Rais wa Marekani Joe Biden huko White House. Bado ni siku za mwanzoni, lakini tunachojua ni kwamba ardhi zaidi ambayo Wa-ukraine wanaweza kuikomboa

Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg alisema Jumanne kwamba msaada wa ushirika wa kijeshi wa Magharibi kwa Ukraine katika vita vyake dhidi ya Russia, sasa unaleta mabadiliko kwenye uwanja wa vita na wakati mashambulizi ya Kyiv ya kulipiza kisasi yakianza.

Mashambulizi yameanzishwa na Wa-ukraine wanapiga hatua, na kusonga mbele, Stoltenberg alisema wakati alipokutana na Rais wa Marekani Joe Biden huko White House. Bado ni siku za mwanzoni, lakini tunachojua ni kwamba ardhi zaidi ambayo Wa-ukraine wanaweza kuikomboa, mkono wenye nguvu zaidi watakuwa nao kwenye meza ya mazungumzo, Stoltenberg alisema na pia uwezekano mkubwa itakuwa kwamba Rais Vladimir Putin katika hatua fulani ataelewa kwamba kamwe hawezi kushinda vita hivi vya uchokozi kwenye uwanja wa vita.

Biden alikubali kwamba NATO kuendelea kuiunga mkono Ukraine kunaleta mabadiliko, akisema kwamba Washirika wa NATO hawajawahi kuwa na umoja Zaidi kama huu, β€œna sisi sote tulifanya kazi bila kuchoka kuhakikisha hilo linafanyika, na hadi sasa tupo katika hatua nzuri sana. Putin anafanya makosa,” alisema Stoltenberg.

Forum

​
XS
SM
MD
LG