Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:03

Moscow huenda inamshikilia Surovikin kuhusiana na uasi wa Wagner


Rais wa Russia Vladimir Putin akimkabidhi tunzo Kanali Jenerali Sergei Surovikin, kamanda wa wanajeshi wa Russia nchini Syria.
Rais wa Russia Vladimir Putin akimkabidhi tunzo Kanali Jenerali Sergei Surovikin, kamanda wa wanajeshi wa Russia nchini Syria.

Maafisa wa usalama wa Russia wanaaminika wanamshikilia Jenerali Sergei Surovikin kwa tuhuma za kuhusika na uasi wa kundi la Wagner wiki iliyopita, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.

Maelezo kamili kuhusu hali ya Surovikin bado hayajulikana, lakini maafisa wa ngazi za juu wa Russia na Marekani wamesema jenerali huyo mkuu yuko kizuizini, magazeti ya Financial Times na The New York Times yameripoti Alhamisi.

Maswali kuhusu mahali aliko Surovikin yamekuwa yakizunguka kwa siku kadhaa kwa sababu ya kutoonekana hadharani kwa jenerali huyo tangu tarehe 24 Juni, wakati kundi la wanamgambo la Wagner lilipokuwa linaelekea Moscow. Surovikin alikuwa akijulikana kuwa na uhusiano mzuri na kiongozi wa Wagner, Yevgeny Prigozhin.

Bado haiko bayana kama Surovikin, naibu kamanda wa kikosi cha uvamizi cha Russia nchini Ukraine, amefunguliwa mashtaka rasmi kwa kuhusika katika uasi huo au amewekwa kizuizini ili kuhojiwa.

Lakini Moscow bado haijathibitisha hadharani nini kilichompata naibu kamanda huyo.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari kwamba hawezi kutoa ufafanuzi kuhusu suala la Surovikin na kuwaambia waandishi wanapaswa kuwasiliana na Wizara ya Ulinzi.

Surovikin alionekana kwenye video siku ya Jumamosi akilisihi kundi la Wagner kusitisha hatua zozote dhidi ya jeshi na kurejea katika vituo vyao.

Binti yake Veronika alisema kuwa "kila kitu kiko sawa" na baba yake. "Kusema kweli, hapana, hakuna kilichompata . Yuko kazini," alliiambia shirika la habari la Russia, Baza.

Prigozhin aliwasili Belarus mapema wiki hii kwa mwaliko wa Rais wa Belarus Alexander Lukashenko ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kusitisha uasi.

Peskov aliwaambia waandishi wa habari Alhamisi kwamba hana taarifa kuhusu kuhusu mahali aliko Prigozhin

Rais wa Marekani Joe Biden alisema Jumatano anaamini kuwa rais wa Russia Vladimir Putin "amedhoofishwa sana" ndani ya Russia na jitihada za uasi za Prigozhin.

Forum

XS
SM
MD
LG