Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 19:05

Ukraine yasema shambulio la kombora la Russia limeua watu tisa katika mji wa Kramatorsk


Mkazi anaitizama nyumba yake iliyoharibiwa na shambulio la kombora la Russia katika mji wa Sloviansk, mkoa wa Donetsk, Aprili 14, 2023.
Mkazi anaitizama nyumba yake iliyoharibiwa na shambulio la kombora la Russia katika mji wa Sloviansk, mkoa wa Donetsk, Aprili 14, 2023.

Maafisa wa Ukraine Jumatano wamesema shambulio la kombora la Russia katika mji wa Ukraine wa Kramatorsk limeua watu 9 na kujeruhi wengine zaidi ya 50.

Huduma za dharura zimechapisha picha za wafanyakazi wa uokoaji wakitafuta masunura chini ya vifusi kwenye eneo ambako pia kuna mgahawa.

Mji wa Kramatorsk upo eneo la magharibi ambako mapigano yanafanyika katika mkoa wa Donetsk mashariki mwa Ukraine.

Shambulio la Russia kwenye kituo cha reli katika mji huo liliua watu 63 mwezi Aprili mwaka 2022.

Ukraine imeripoti pia kwamba shambulio la kombora la Russia jana Jumanne katika mji wa Kremenchuk liliua watu 20 kwenye jengo la maduka.

Forum

XS
SM
MD
LG