Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:38

Marekani yalaumu makampuni yanayoshirikiana na kundi la Wagner


Picha ya mamluki wanaodaiwa kutoka kundi la Wagner la Russia wakiwa kaskazini mwa Mali.
Picha ya maktaba.
Picha ya mamluki wanaodaiwa kutoka kundi la Wagner la Russia wakiwa kaskazini mwa Mali. Picha ya maktaba.

Marekani Jumanne imelaumu baadhi ya makampuni kutoka Umoja wa falme za Kiarabu UAE, Jamhuri ya Afrika ya Kati  pamoja na serikali ya Russia kwa kujihusisha kwenye biashara haramu ya dhahabu ili kufadhili kundi la mamluki kutoka Russia la Wagner.

Taarifa ya wizara ya fedha ya Marekani imesema kwamba Marekani imeweka vikwazo kwa makampuni 4 yanayohusishwa na Wagner pamoja na kiongozi wake Yevgeny Prigozhin, yakidaiwa kutumika kulipa vikosi vya kundi hilo vinavyopigana Ukraine, pamoja na kuongoza operesheni zinazozingatia maslahi ya Russia barani Afrika.

Brian Nelson ambaye ni naibu waziri wa fedha wa Marekani kupitia taarifa hiyo ameongeza kusema kwamba kundi la Wagner linafadhili operesheni zake kwa kuiba mali asili kwenye mataifa kama Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na Mali. Ameongeza kusema kwamba Marekani itaendelea kulenga vyanzo vya fedha vya kundi hilo, ili kudumaza shughuli zake barani Afrika, Ukraine na kwingineko.

Forum

XS
SM
MD
LG