Fedha hizo zitatumika kusaidia biashara na raia kuendeleza shughuli za uzalishaji kufuatia athari za janga la virusi vya corona kwenye uchumi wa nchi hiyo.
Katika hotuba yake, rais Kenyatta amesema pesa hizo zitatolewa katika sekta muhimu kama vile miundo mbinu, elimu, biashara ndogo ndogo na za wastani, afya, kilimo, utalii, mazingira na viwanda.
Ameongeza kuwa Kenya haiwezi kuendelea kuwa chini ya masharti ya kufunga shughuli zote na amri ya kutotoka nje usiku milele.
Matamshi yake yanashabihiana na yale ya wakazi wengi katika maeneo yaliyoathiriwa wanaochukulia kwamba serikali haikutilia maanani shughuli zao za kiuchumi au kuwapatia njia mbadala ya kukidhi maisha yao.
Baadhi ya watu wametaka amri hiyo ya kutotoka usiku iangliwe upya na kusema ianze saa tatu usiku badala ya saa moja usiku.
Amesema serikali imeendelea kutoa shilingi milioni 250 kila wiki kusaidia familia zenye matatizo ambazo zimeathiriwa na virusi na mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini.
“Janga hilo limekuwa na athari hasi kwa uchumi wa Kenya ambapo watu wengi wamevuliwa ubinadamu wao na kuathiriwa vipato vyao, hadi kufikia hali ya kushindwa kuzipatia familia zao chakula na kulipa kodi.” Amasema Kenyatta
Rais Uhuru amesema serikali imechagua kuwapelekea familia hizo zilizoathiriwa fedha kutokana na kupotea kwa zaidi ya nusu ya msaada waliokuwa wamepeleka kwa familia zilizofikiwa na majanga, huko siku za nyuma.
Mchakato huu, umesaidia kuwadhibiti watu wa kati na matapeli ambao walikuwa wanatawalia sekta hii ya misaada,” Rais Uhuru.
Jambo la pili, serikali imeweza kufufua uchumi wa maeneo kupitia fedha zilizopelekwa kwa familia hizo ambazo ni kiwango cha shilingi milioni 250 kila wiki.
“Fedha zikiwa mikononi mwa familia zinarejesha ubindamu wao kwani huwapa uwezo watu wa kufanya maamuzi ya kiuchumi katika hali zao na siyo kusubiri kupanga foleni wakisubiri vyakula vya msaada – Hii inatusaidia kujenga uchumi kutoka chini kwenda juu,” amesema Rais Kenyatta.