Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:05

Kenya yaongeza muda wa katazo la kutoka nje usiku


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Serikali ya Kenya Jumamosi ilitangaza hatua ya kuongezewa kwa muda wa katazo la kutoka nje usiku, kwa siku zingine 21 kama mojawapo ya njia za kupambana na janga la Corona baada ya kipindi cha kwanza cha katazo hilo kumalizika.

Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, katika hotuba yake kwa taifa, alisema kuna umuhimu wa kuongeza muda huo, ili kupunguza athari ya kuongezeka kwa kasi kwa maambukizi ya homa hiyo hatari.

Aidha Kenyatta alitangaza hatua zingine mpya za kukabilina na janga hilo.

Marufuku ya usafiri - Kutoka au kuingia katika majimbo ya Nairobi, Kwale, Mombasa na Kilifi - pia iliongezwa muda kwa siku 21.

Kenyatta alitaja majimbo ya Kwale na Mandera kama yaliyoshuhudia ongezeko kubwa la maambukizi ya Corona, lakini akaongeza kwamba kwa ujumla, hatua ambazo zimechukuliwa na serikali yake zimesaidia pakubwa kuzuia idadi ya maambukizi kupand zaidi.

Wakati huo huo, rais huyo alikanusha ripoti zilizochapishwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba Kenya itatumiwa kwa majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

"Hakuna ukweli kuhusu hilo. Nijuacho ni kwamba taasisi zetu za utafiti kam vile KEMRI zinashirikiana na taasisi za kimataifa kutafuta suluhisho," alisema Kenyatta.

"Msiamini habari za kupotosha," aliongeza.

Hadi tulipokuwa tukitayarisha ripoti hii, Kenya ilikuwa na visa 343 vya maambukizi vilivyothibitishwa, huku watu waliokufa kutokana na ugonjwa huo wakifikia 14.

Hata hivyo, nchi hiyo imeripoti kwamba watu 98 wamepona ugonjwa huo. Marufuku hiyo ya kutoka nje usiku, ambayo inaanza saa moja jioni, awali ilizua sintofahamu, na kupelekea makabiliano makali kati ya raia na maafisa wa kulinda usalama.

XS
SM
MD
LG