Hayo ni kwa mujibu wa nyaraka rasmi zilizowasilishwa katika mahakama ya Chicago, Marekani Jumatano. Kampuni hiyo imesema Boeing ina nia ya dhati kuhakikisha familia zilizopoteza wapendwa wao kwenye ajali hiyo wanalipwa fidia kwa haki.
Ndege 302 iliyokuwa inakwenda Nairobi, Kenya inayomilikiwa na shirika la ndege la Ethiopia ilianguka kusini mashariki mwa mji mkuu wa Addis Ababa dakika sita baada ya kupaa Machi mwaka 2019.
Ajali hiyo ilisababisha kusitishwa kwa ndege aina ya 737 MAX na kupelekea mzozo mkubwa duniani katika historia ya utengenezaji wa ndege Marekani wakati tukio lilitokea baada ya ndege nyingine 737 MAX iliyokuwa inamilikiwa na shirika la Lion kuanguka Indonesia mwezi Oktoba mwaka 2018 na kuuwa watu 189 waliokuwemo ndani.
Mawakili wa familia zilizoathiriwa walifikia makubaliano hayo ya kihistoria katika kutafuta haki dhidi ya kampuni ya Boeing.