Kamati ya usafiri na miundo mbinu katika bunge la Marekani siku ya Jumanne ilimtaka rasmi mkurugenzi huyo kutoa ushahidi juu ya ndege aina ya 737 MAX ambayo hivi sasa imezuiliwa kusafiri kutokana na ajali mbili zilizosababisha vifo vya watu 346 tangu Oktoba mwaka jana.
Mwenyekiti wa kamati hiyo mbunge Peter DeFazio pia alimtaka John Hamilton mkuu wa uhandisi katika kitengo cha biashara cha Boeing kufika bungeni kutoa ushahidi wake. Wawili hao wanatakiwa kufika bungeni Oktoba 30 mwaka huu.
Wiki iliyopita DeFazio alimuomba Muilenburg kuwatayarisha wafanyakazi kadhaa wa kampuni hiyo kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano kama sehemu ya uchunguzi wa bunge la Marekani kuhusiana na namna ndege hiyo ilivyotengenezwa, maendeleo pamoja na utendaji kazi wa ndege hiyo aina ya 737 MAX.