Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:48

Idadi ya waliokufa kutokana na kimbunga Dorian yafikia 43 Bahamas


Mwanamke akitafuta miili ya familia yake iliyotoweka kutokana na kimbunga Dorian katika kifusi cha nyumba yake huko High Rock, Grand Bahama, Bahamas, Sept. 6, 2019.
Mwanamke akitafuta miili ya familia yake iliyotoweka kutokana na kimbunga Dorian katika kifusi cha nyumba yake huko High Rock, Grand Bahama, Bahamas, Sept. 6, 2019.

Timu za waokoaji bado zinajaribu kuwatafuta na kuzifikia jamii za watu wa Bahamas ambao wametengwa na mafuriko na vifusi vya nyumba zao baada ya kimbunga Dorian kupiga eneo hilo.

Wakati huohuo idadi ya watu waliokufa katika janga hilo wamefikia 43 na kunauwezekano wa kuongezeka zaidi, maafisa wa ngazi ya juu wamesema.

Waziri wa Afya Duane Sands amesema jioni siku ya Ijumaa katika ujumbe wa maandishi aliyopeleka shirika la habari la AP kuwa vifo zaidi 13 vimethibitishwa mbali ya vile 30 vya hapo awali.

“Tunategemea idadi hiyo kuongezeka,” amesema Sands.

Waziri wa Usalama Marvin Dames amesema vyombo vya usalama bado vinafanya bidi ya kumfikia kila mtu, lakini timu hizo haziwezi kusonga mbele kutokana na vizuizi vya miti iliyoanguka na vifusi vingine kwa sababu inawezekanakuna miili ambayo bado haijagunduliwa.

“Tumewahi kupitia janga kama hili siku za nyuma, lakini siyo katika kiwango hiki cha uharibifu,” Dames amesema. “Huku ni wakati mgumu sana na pia hali tete sana.

Hata hivyo amesema anaelewa kwa nini wananchi wanalalamika ambao wanapaza sauti kuomba msaada baada ya maisha yao kuharibika kutokana na kimbunga Dorian, lakini alitoa wito watu wawe wavumilivu wakati serikali ilifanya juhudi ya kuwafikishia msaada wa dharura.

“Hakuna kinachoweza kufanyika kwa siku moja. Hisia kwamba juhudi za haraka lazima zifanyike ni kawaida, ‘Tupelekeni kila kitu kinachohitajika mara moja,’ lakini ukweli ni kwamba unaweza tu ukapeleka msaada wa kiwango fulani kwa wakati mmoja,” amesema.

Juhudi za kutafuta wahanga na walionusurika ziliendelea kwa siku tano baada ya kimbunga Dorian kupiga Bahamas. Kimbunga hicho kilikuwa kinasafiri maili 185 (kilomita 295) kwa saa ambacho kiliangamiza nyumba zisizo kuwa na hisabu. Maafisa wanasema watu 43 wamethibitshwa kupoteza maisha lakini walitahadharisha kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Taasisi, nchi na makampuni mbalimbali, ikiwemo Umoja wa Mataifa, Serikali ya Marekani, Jeshi la Ufalme wa Uingereza, Shirika la ndege la American Airlines, Ufalme wa Caribbean, kwa pamoja wamepeleka chakula, maji, majenereta, vifaa vya kuezeka nyumba, tochi na mahitaji mengineyo. Seneta wa Marekani Marco Rubio wa Florida amesema Shirika la misaada la Marekani limeitaka Wizara ya Ulinzi kutoa ndege zenye uwezo wa kubeba mizigo mizito ili kupeleka mahitaji hayo Bahamas.

XS
SM
MD
LG