Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 04:33

Mvua, kimbunga nchi za Pembe ya Afrika zauwa watu 20


Ramani ya Somaliland and Puntland
Ramani ya Somaliland and Puntland

Watu wasiopungua 20 wameuwawa na wengine hawajulikani waliko baada ya mvua kubwa iliyosababishwa na upepo mkali kunyesha nchi za Pembe ya Afrika.

Watu 15 waliuwawa katika mkoa wa Awdal katika eneo lililojitangazia mamlaka ya kujitawala la Somaliland kwa mujibu wa gavana wa mkoa huo Abdirahman Ahmed Ali, na mtu mwengine aliuwawa na kimbunga hicho katika mji wa Berbera katika mkoa wa Sahil.

Ali amesema kuwa ripoti hiyo bado ni ya awali na idadi ya waliokufa katika kimbunga hicho inaweza kuongezeka wakati wakijaribu kufikia maeneo yaliombali katika mkoa ulioathiriwa na mvua hizo kubwa.

Wengi waliokufa katika tukio hilo walikumbwa na mafuriko hayo, wakazi wameeleza.

Wakazi wa mji wa Baki katika mkoa wa Awdal wamesema kuwa watu wanne walipoteza maisha ambapo kati yao watatu waliuwawa katika mafuriko hayo na wanne aliangukiwa na nyumba.

Mohamed Aw Ahmed Ateye ni mkuu wa baraza la wilaya katika mji wa Baki.

“Kuna hasara kubwa sana ya watu kupoteza maisha na mali nyingi kuangamia,” ameiambia Sauti ya Amerika VOA.

Serikali za eneo hilo zimeripoti kuwa mamia ya mifugo ikiwemo kondoo, mbuzi na ngamia waliuwawa kutokana na mvua hizo zilizoambatana na mafuriko na kimbunga kikali. Katika eneo karibu na Baki, maafisa wameripoti kulikuwa na kondoo na mbuzi 340 waliokufa na ngamia 26.

Katika Kijiji cha karibu cha Qardhile, mkulima Mohamed Abdi Farah ameiambia VOA kuwa kati ya kondoo na mbuzi wake 184, 20 tu ndio walionusurika.

Ateye ameripoti kuwa nyumba 41 zilibomoka kutokana na mafuriko hayo katika mji huo, na nyengine 30 ziliharibiwa kabisa katika mji wa Harirad. Pia amesema kuwa mashamba 140 yameangamizwa wakati ambapo mafuriko hayo yakiharibu mazao.

“Mafuriko hayo yameharibu mazao, vifaa vya mashambani na madaraja yamesombwa na maji baada ya mvua hiyo kubwa kudumu kwa masaa 17,” amesema.

XS
SM
MD
LG