Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:11

Baraza la Usalama lataka nchi wanachama kuongeza juhudi kukabiliana na tishio la hali ya hewa


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Katika  mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Juni, wazungumzaji waliyasihi mataifa wanachama kufanya mengi zaidi kukabiliana na tishio la usalama linaloletwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Wakati huo huo, nchini Chad, mizozo kati ya wakulima wafugaji kutoka kabila la Fulani inazidi kuongezeka wakati hali ya viwango vya joto vikizidi kupunguza maji ambayo tayari ni adimu kupatikana na hakuna ardhi ambayo inaweza kutumika.

Katika maeneo ya nje ya mji mkuu wa Chad, N’Djamena, wakulima na wafugaji wanasema wameona mabadiliko ya hali ya hewa katika miaka ya karibuni. Imekuwa ni vigumu sana kulima, huku mvua zikiwa chache na viwango vya joto vikiwa juu mno.

Umoja wa Mataifa unasema ardhi ambayo inaweza kutumiwa na wakulima na wafugaji inazidi kupungua, hali inayozidisha mzozo kati ya makundi hayo.

Wakulima kama Abdelaziz Mahamat anasema imekuwa ni muhimu kujenga uzio wenye urefu wa kiasi cha mita mbili ili kulinda mazao yake yasivamiwe na ngo’mbe.

“Tunajenga uzio kuwazuia wezi na wanyama wanaozurura kuingia mashambani. Changamoto kubwa sana ni kuwepo kwa ng’ombe wanaozagaa tu. Wafugaji wamejihami kwa visu na silaha,” anasema Abdelaziz Mahamat.

Watalaamu wanasema kwamba mzozo wa wafugaji na wakulima, ambao umekuwa mbaya zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, umehusishwa na ukosefu wa usalama katika eneo la Sahel katika miaka ya karibuni.

Wengi kutoka pande zote wanaonekana hawafahamu athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa maisha yao na badala yake wanamuangalia mwenyenzi mungu kuwapatia suluhisho.

Haroun Bechara, kiongozi wa jamii ya wafugaji Kiongozi wa Jamii ya Wafugaji anasema,“sifahamu nini hasa kinasababisha matatizo haya ya hali ya hewa hapa. Kwa kweli tunahitaji mvua. Ndiyo, tunasali kumuomba mungu kila siku na kumuomba atupatie maji. Hicho ndiyo tunaweza kukifanya.”

Katika miaka ya karibuni, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilianza kujadili jinsi linavyoweza kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa katika muktadha wa kuhamasisha utulivu.

Janani Vivekananda, mkuu wa program ya Diplomasia na Usalama wa Hali ya Hewa huko Adelphi, kampuni ya ushauri yenye makao yake Berlin, anaelezea jinsi baraza linavyoweza kupitisha azimio linaloshughulikia jinsi ya kukabiliana na tatizo hili.

Hivi karibuni, serikali ya Mali iliiomba tume ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa kuondoka nchini humo, baada ya kushindwa kupunguza ghasia ambazo zinaaminika kusababishwa kwa kiasi na hali ya joto joto duniani.

Vivekanda anasema “nadhani Mali, kwa bahati mbaya, ni mfano mzuri wa jinsi majeshi ya ulinzi wa amani na utulivu hayajaweza kukidhi lengo, kwasababu kwa njia ambayo athari za mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha mzozo, kuelewa kiini cha sababu za mzozo, mabadiliko ya hali ya hewa kumedumaza tayari maisha ya watu ambayo tayari yamekumbwa na ugumu.”

Watalaamu wanasema ukosefu wa usalama umesababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na mapigano juu ya rasilimali kama vile maji na ardhi na hali yatakuwa mbaya zaidi.

Florian Krampe, wa taasisi ya kimataifa ya utafiti wa amani huko Stokcholm anasema, “tuna picha ya dhahiri kwamba mambo mengi yanayohusu usalama kama ghasia, vurugu za kijamii zinahusishwa na matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa. Wao ni sehemu ya hadithi.”

Ameongezea, “Hili ni tatizo la leo……na ni tatizo ambalo litazidi kuongezeka”


Forum

XS
SM
MD
LG