Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:38

Usambazaji wa misaada ya kibinadamu huko Syria huwenda ikaongezewa muda


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres

Uidhinishwaji wa hivi sasa wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa usambazaji wa misaada  kupitia njia ya Bab al-Hawa unatarajiwa kuisha muda wake Jumatatu, lakini baraza hilo lina maazimio mawili ya kuongeza muda kabla ya kupiga kura

Usambazaji wa misaada ya kibinadamu kwa eneo linaloshikiliwa na waasi huko kaskazini magharibi mwa Syria kutokea nchi jirani ya Uturuki kuna uhakika wa kupata ruhusa ili kuendelea kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lakini swali linaloibuka, ni kwa muda gani.

Uidhinishwaji wa hivi sasa wa baraza hilo kwa usambazaji wa misaada kupitia njia ya Bab al-Hawa unatarajiwa kuisha muda wake Jumatatu, lakini baraza hilo lina maazimio mawili ya kuongeza muda kabla ya kupiga kura.

Azimio la Russia litaendelea kutoa misaada kwa miezi sita, na azimio la Brazil na Uswisi linaloungwa mkono na wanachama wengi wa baraza hilo paamoja na Katibu Mkuu Antonio Guterres litaidhinisha kuongezwa kwa muda wa miezi 12. Upigaji kura huo ulikuwa umepangwa kufanyika Jumatatu asubuhi lakini uliahirishwa.

Brazil, Uswisi na Umoja wa Falme za Kiarabu zinatafuta muafaka na Russia juu ya muda uliopangwa na kura inaweza kufanyika wiki hii, wanadiplomasia walisema, wakizungumza kwa sharti la kutotajwa jina kwa sababu majadiliano yamekuwa ya faragha.

Forum

XS
SM
MD
LG