Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:51

Syria itairuhuusu UN kutumia mpaka wake na Uturuki kutoa misaada ya kibinadamu


Bango la barabarani linalosomeka "Karibu kwenye mpaka wa Bab al-Hawa" (Welcome to Bab al-Hawa) katika mpaka wa Syria na Uturuki. Syria, June 10, 2021.
Bango la barabarani linalosomeka "Karibu kwenye mpaka wa Bab al-Hawa" (Welcome to Bab al-Hawa) katika mpaka wa Syria na Uturuki. Syria, June 10, 2021.

Serikali ya Jamhuri ya Kiarabu ya Syria imechukua uamuzi wa kuipa Umoja wa Mataifa na mashirika yake maalum ruhusa ya kutumia njia ya Bab al-Hawa, kupeleka misaada ya kibinadamu kwa raia wenye shida  kaskazini magharibi mwa Syria

Syria imesema itauruhusu Umoja wa Mataifa kutumia kwa muda mpaka wake na Uturuki kuwafikia mamilioni ya raia wa Syria wanaoishi katika maeneo yaliyo nje ya udhibiti wa serikali.

Serikali ya Jamhuri ya Kiarabu ya Syria imechukua uamuzi wa kuipa Umoja wa Mataifa na mashirika yake maalum ruhusa ya kutumia njia ya Bab al-Hawa, kupeleka misaada ya kibinadamu kwa raia wenye shida kaskazini magharibi mwa Syria, kwa ushirikiano kamili na uratibu na serikali ya Syria kwa kipindi cha miezi sita, kuanzia Julai 13, 2023,” Balozi Bassam al-Sabbagh aliwaambia waandishi wa habari katika Umoja wa Mataifa.

Matumizi ya mpaka wa Bab al-Hawa kutoka Uturuki kuelekea kaskazini magharibi mwa Syria yamekuwa ya kutatanisha. Serikali ya Bashar al-Assad inataka misaada yote ipitie Damascus na kuvuka mipaka ya mgogoro kutoka ndani ya Syria.

Mshirika wake Russia ilitumia kura yake ya turufu katika Baraza la Usalama siku ya Jumanne kuzuia kuongezwa kwa miezi tisa, kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhamisha usafirishaji wa misaada ya kibinadamu kupitia Bab al-Hawa.

Forum

XS
SM
MD
LG