Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:01

Palestina yasema jeshi la Israel limewaua Wapalestina wanane Ukingo wa magharibi


Moshi watanda kufuatia shambulio la Israel, huko Khan Younis kusini kwa ukanda wa Gaza, Mei 9, 2023.
Moshi watanda kufuatia shambulio la Israel, huko Khan Younis kusini kwa ukanda wa Gaza, Mei 9, 2023.

Maafisa wa afya wa Palestina wamesema wanajeshi wa Israel wamewaua watu wanane leo Jumatatu katika shambulizi katika eneo linalokaliwa kimabavu huko ukingo wa magharibi.

Jeshi la Israel limesema liliendesha shambulio katika kambi ya wakimbizi ya Jenin, na kushambulia kile ilichokiita “kituo cha uongozi wa pamoja” wa wanamgambo.

Jeshi la Israel limetumia pia ndege zisizo na rubani katika mashambulizi hayo.

Msemaji wa jeshi la Israel, kanali Richard Hecht amesema wanajeshi wa Israel walikamata silaha na risasi.

Wizara ya afya ya Palestina imesema watu 27 walijeruhiwa pia.

Israel imeendesha mashambulizi ya mara kwa mara katika eneo hilo, likiwemo shambulio la mwezi uliopita lililoua Wapalestina saba.

Wiki iliyopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliomba pande zote kujizuia na ghasia na kuwataka Waisraeli na Wapalestina kujiepusha na vitendo vya upande mmoja ambavyo vinaweza kuchochea mivutano zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG