"Port-au-Prince imezingirwa na makundi yenye silaha ambayo yanafunga barabara, kudhibiti upatikanaji wa chakula, na huduma za afya, na kudhoofisha msaada wa kibinadamu," alisema kuhusu mji mkuu, ambao alitembelea hivi karibuni.
Guterres aliwaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kwamba Haiti inahitaji usaidizi wa kibinadamu na kiusalama, pamoja na njia ya kisiasa ya kujiondoa katika mgogoro huo.
Oktoba mwaka jana, serikali ya Haiti iliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha kikosi cha kimataifa, kusaidia vikosi vya polisi wa kitaifa, katika kuondoa tishio kutoka kwa magenge, ambayo yanatishia watu na kuwazuia kupata chakula, maji safi, elimu na huduma nyingine za kimsingi.
Polisi pia wanahitaji fedha, mafunzo na vifaa, ili kurejesha mamlaka, na huduma za serikali. Lakini miezi tisa baadaye, Baraza la Usalama haliko karibu na kuidhinisha jeshi na hakuna nchi iliyojitokeza kuliongoza. Waziri wa mambo ya nje wa Haiti, Jean Victor Geneus, alifika mbele ya baraza hilo siku ya Alhamisi, na kusisitiza udharura wa wito wa serikali.
Forum