Miongoni mwa waliotoweka ni Faraj Abderrahmane Boumtari, waziri wa zamani wa fedha.
Siku ya Jumatano, Boumtari “aliripotiwa kukamatwa katika uwanja wa ndege wa Mitiga na kupelekwa katika eneo lisilojulikana”, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) ulisema katika taarifa. Taarifa hiyo imeongeza kuwa “wanachama watano wa Baraza Kuu la Taifa wameripotiwa kupigwa marufuku kusafiri katika uwanja huo huo wa ndege”, mjini Tripoli.
UNSMIL imeonya kuwa vitendo kama hivyo vinasababisha “hali ya hofu, kuongeza mivutano kati ya jamii na makabila, na kuwa na athari kubwa kwa umoja wa taasisi za kitaifa”.
Forum