Kufikia sasa rais Kenyatta anaongoza kwa Zaidi ya kura milioni 7.2. Uchaguzi huo wa urais, ambao umezua utata, ulifanyika siku ya Alhamisi licha ya mgombea wa upinzani, Raila Odinga, kujitoa kwenye kinyang’anyiro hicho, kwa madai kwamba haungekuwa wa haki na wa kweli.