Tume ya uchaguzi na mipaka Kenya - IEBC imetangaza matokeo hayo na kusema kuwa amepata zaidi ya asilimia 98 ya kura.
Idadi ya watu waliojitokeza kwenye uchaguzi wa marudio wa wiki iliyopita ilikuwa chini ya asilimia 39 ya wapiga kura milioni 19.6 waliojiandikisha, alisema Wafula Chebukati, mwenyekiti wa tume huru na mipaka Kenya-IEBC.
Kiongozi wa muungano wa upinzani, Nasa, Raila Odinga ambaye alijitoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wa marudio alitoa wito kwa wafuasi wake kususia upigaji kura huo na waandamanaji walizuia vituo vya kupiga kura kufunguliwa katika baadhi ya ngome za upinzani.
Upigaji kura wa Oktoba 26 ulikuwa ni uchaguzi wa marudio wa urais uliofanyika Agosti nane ambapo Kenyatta alitangazwa mshindi, lakini matokeo yalitenguliwa baadae na mahakama ya juu ya Kenya kwa sababu ya kasoro zilizojitokeza.