SIiku ya Jumapili polisi nchini humo walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliokuwa wanaandamana mjini Nairobi kupinga mauaji ya watu wanne yaliyotekelezwa jaJumamosi usiku katika mtaa mmoja wa mabanda mjini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, baadhi ya mitaa ya mji huo imekumbwa na hali ya taharuki tangu Ijumaa, wakati takriban watu watano waliuawa kufuatia makanbiliano kati ya polisi na wafuasi wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, ambaye alikuwa amerejea kutoka ziarani Marekani.
Polisi hata hivyo wamesema waliouawa ni wahalifu.
Haya yamejiri siku moja tu kabla ya mahakama ya juu ya Kenya kutoa uamuzi wake kufuatia kesi zilizowasilishwa kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa tarehe 26 mwezi jana.
Jaji mkuu David Maraga ametangaza kwamba uamuzi huo utatolewa saa tano asubuhui siku ya Jumatatu.