Radio
Rais wa Ghana na mawaziri wake wajipunguzia mishahara yao kwa asilimia 30
Rais wa Ghana Nana-Akufo Addo na mawaziri wake wamepunguza mishahara yao kwa kiwango cha asilimia 30 kama hatua za kupunguza matumizi ya serikali, wakati nchi inakabiliwa na gharama kubwa za mafuta kutokana na mzozo wa Ukraine na kukwama kwa mswada wa sheria kuhusu kodi mpya.
Serikali ya Kenya yatangaza kwamba watu milioni 2.8 wanakabiliwa na njaa.
Watu milioni 2.8 wanakabiliwa na mahitaji ya chaklula ya haraka katika kaunti 23 hii ikiwa ni ongezeko la kutoka watu milini 2.1 waliokabiliwa na njaa mwezi Septemba mwaka jana.Kaungti ambazo zinaathrika zaidi ni Baringo, Isiolo, Mandera,Marsabit, Samburu, Turkana na Kilifi.
Rais Joe Biden awasili Poland ambapo ni kituo chake cha mwisho cha ziara yake
Katika habari za Dunia: Rais Joe Biden wa Marekani awasili Poland ambapo ni kituo chake cha mwisho cha ziara yake. Live Talk: Kwa nini mataifa ya Afrika Mashariki na Kati yamekuwa tegemezi kwa mazao ya chakula kutoka mataifa ya nje, kwa sasa ikiwa ni Ngano kutoka Ukraine na Russia zikiwa vitani.
Waandishi wajadili habari kuu za wiki katika 'Jukwaa la Waandishi'
Waandishi Mary Mgawe, Jackline Odhiambo na Ali Mtasa wanaangazia ripoti mbalimbali zilizogonga vichwa vya habari kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, zikiwa ni pamoja na Mzozo wa wakimbizi nchini Ukraine, Mkutano wa dharura wa NATO na maadhimisho ya Siku ya Maji Duniani.