WHO yagundua namna kirusi corona kinavyoambukiza

Mkutano wa wanasayansi na wataalam wa afya nchini Geneva uliojadili maambukizo ya kirusi corona, Geneva, Switzerland, Februari 11, 2020.REUTERS/Denis Balibouse

Wanasayansi na wataalamu kutoka taasisi za afya za kimataifa waliokutana kwenye makao makuu ya Shirika la Afya Duniani, WHO, mjini Geneva, wanasema wamegundua jinsi kirusi corona kinavyoambukizwa.

Wataalamu hao waliokutana kujadili namna ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa unaosababishwa na kirusi corona, wanasema kipaumbele chao hivi sasa ni kuvitambua zaidi virusi hivi tabia zake, asili yake na jinisi vinavyo ambukiza watu kutoka kwa wanyama.

Wakati hayo yakitangazwa maafisa wa afya wa China wanasema wamepokea ripoti za idadi mpya ya watu 15,152 walioambukizwa upya na kirusi hicho, mbali na wale elfu 13 332 katika jimbo la Hubei.

Maafisa wanasema idadi hiyo mpya ni ya watu katika wilaya na majimbo mengine 31 ya China na idadi ya walofariki imefikia 1 367.

Hayo yakiendelea meli ya utali iliyokua baharini kwa wiki mbili baada ya kukataliwa nan chi tano kutia nan’ga imekubaliwa kuingia Cambodia hii leo. Abiria 1 455 na wafanyakazi 802 katika meli ya MS Westerdam walikua na furaha nyingi meli ilipokua inatia nan’ga katika bandari ya Sihanoukville.

Na huko Yokahoma Japan maafisa wa afya wamewaruhusu baadhi ya abiria ambao hawakuambukizwa na virusi vya Corona kushuka kutoka meli nyingine ya utaliya Dimond Princess. Nahodha wa meli hiyo alitangaza watu wengine 44 wameambukizwa na kufikisha idadi ya wagonjwa ndani ya meli hiyo kua 218.