Polisi nchini Madagascar wamewakamata watu kadhaa ambao wanaamini walikuwa sehemu ya njama ya kumuua Rais Andry Rajoelina.
Ofisi ya mwanasheria mkuu ilitoa taarifa Alhamisi ikisema washukiwa walikuwa sehemu ya njama ya kudhoofisha usalama wa taifa wa kisiwa hicho, pamoja na kutokomeza watu kadhaa.
Washukiwa hao ni pamoja na raia wa kigeni na raia waliozaliwa nchini Madagascar. Taarifa hiyo ilisema uchunguzi bado unaendelea.