Nao wabunge wa Chama Cha Republican wanalaani mashambulizi ya Hamas wakisema huwezi kulinganisha kwa usawa vitendo vya pande hizo mbili.
Ghasia zinazoendelea kati ya Wapalestina na Israel
Kundi la Hamas kwa siku 10 mfululizo limekuwa likifyatua roketi ndani ya Israel katika kile wapiganaji wake wanasema ni ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa dhidi ya Wapalestina, huku Israel ikijibu kwa mashambulio ya anga kwenye ukanda wa Gaza.
Chris Murphy Seneta Mdemokrat anasema Israeli ilifanya makoso kuendelea na mpangio wa kujenga makazi na kuwaondowa Wapalestina ikiwa ni kama njia ya makusudi ya kuhujumu taifa la baadae la Palestina.
Seneta Murphy anaeleza : "Sera hizi huenda zikasaidia kuunganisha pamoja Netanyahu na muungano wake wa kisiasa, lakini zimesaidia kuchochea hali ya kutokuwa na matumaini miongoni mwa Wapalestina na mustakbali wao. Uongozi wa Wapalestina ulifanya pia makoso kwa kueneza Wazi chuki dhidi ya Israeli kama msingi wake wa kubaki madarakani."
Msimamo wa Wademokrat Kuhusu Mageuzi
Wademokrats wanaopendelea mageuzi, wenye msimamo mkali wa kushoto akiwemu Seneta Bernie Sanders na Mbunge Alexandria Ocasio Cortez wanatoa wito kutathmini upya msaada wa Marekani kwa Israel kwa sababu ya majeruhi ya kiraia yanayosababishwa na mashambulio ya anga ya Israel.
Lakini wabunge wengi wenye msimamo wa wastani wanatoa wito wa kusitishwa mapigano. Seneta Bob Menendez Mdemokrat anasema juhudi za kidiplomasia zinaendelea.
Seneta Menendez : Wote waziri Blinken na rais binafsi wanajihusisha kikamilifu katika juhudi za kidiplomasia za chini kwa chini, za moja kwa moja na serikali ya Israel na Misri pamoja na washirika wengine katika kanda hiyo ili kuweza kukomesha mapigano hayo.
Warepublican kwa upande wao wanasema huwezi kulinganisha wajibu wa pande zote mbili. Seneta wa walio wachache kwenye baraza la Seneta Mitch McConnell anahisi Wademokrat wanawalaumu Waisrael hivi sasa.
McConnel awashutumu Wademokrat
McConnell aeleza : Kuna idadi kubwa ya Wademokrat wanataka kuwalaumu Waisrael na kujifanya kuna usawa wa majukumu. Hakuna usawa wa kimaadili, kundi la kigaidi upande mmoja linalowatumia kwa hakika Wapalestina kwa faida zao binafsi kwa kuwaweka hatarini mara kwa mara, na huku Waisraeli wakilenga shabaha zao ili kulinda nchi yao.
Wito wa Warepublikan
Masemeta Warepublican wanatoa wito wa kuchukuliwa hatua zaidi kuilinda Israeli, kwa kuongeza msaada wake wa kijeshi wakati wakilaani hatua ya utawala wa Biden kujiunga na mkataba wa Nyuklia na Iran.
Na wakati huo huo utawala wa Biden ukikabiliwa na changamoto kutoka Wademokrat wapenda mageuzi wanaotaka kuzuia biashara ya silaha yenye thamani ya dola milioni 735 kwa Israel. Muda wa kukamilisha mkataba huo umeshakaribia, hakuna dalili za kuweza kuuzia kutekelezwa.