Vyama vyenye kukosoa EU vyaongoza Uingereza, Ufaransa na Italia

Wapiga kura wakisubiri katika vituo vya kupiga kura katika kuchagua wabunge wakuwakilisha nchi yao Umoja wa Ulaya mjini Dresden, Ujerumani, Mei 26, 2019.

Vyama ambavyo vimekuwa vikiikosoa Umoja wa Ulaya vinaongoza kwenye kura katika uchaguzi wa bunge la umoja huo nchini Uingereza, Ufaransa na Italia.

Vyama hivyo katika nchi 28 wanachama wa Umoja huo vinaonekana kuongoza kwenye uchaguzi ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano na kwa hivyo kuongeza viti vyao kwenye bunge la wajumbe 751 kutoka 155 hadi 169.

Chama cha Mateo Savini cha Lega nchini Italy kimepata ushindi mkubwa kikielekea kujipatia karibu basilimia 30 ya kura nchini humo ambapo Savini amesema kuwa wapiga kura wamempa nafasi ya kihistoria ya kuibadilisha Umoja wa Ulaya.

Wakati huo huo Savini amempongeza Marine Len Pen kutokana na ushindi wa chama chake dhidi ya chama cha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macro cha En Marche pamoja na ushindi wa chama kipya cha Brexit chini ya uongozi wa Nigel Farage nchini Uingereza.

Amesema kuwa hatimaye wataweza kuikomboa Ulaya kutokana na miongo mingi ya uongozi wa kibepari na sheria za wenye mabenki.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.