Jumuiya ya tafiti za vyombo vya Habari na Sheria, taasisi isiyokuwa ya kibiashara ya Uturuki, imesema itapinga amri hiyo. Kikundi hicho kimesema sheria hizo mpya zinakandamiza haki na uhuru wa kujielezea, kupata habari na kueneza habari.
Jambo ambalo halifahamiki ni jinsi gani sheria hizi zitaathiri matangazo ya mtandao wa Netflix, idhaa ya BBC, Sauti ya America (VOA) na mashirika ya habari na burudani ambayo yanatangaza maudhui yake kupitia intaneti na simu nchini Uturuki.
Muhtasari wa sheria hizo zilizochapishwa na kampuni ya kimataifa ya Baker McKenzie inaeleza sheria hizo zitawagusa watoa huduma wa nje ambao “wanarusha maudhui kupitia intaneti kwa lugha ya Kituruki inayowalenga Watu wa Uturuki.
Netflix ilotoa tamko ikisema kampuni hiyo inafuatilia kwa karibu sheria hii. “Netflix ina washabiki wanaoongezeka nchini Uturuki, ambao wanathamini mchanganyiko wa maudhui ambao unapatikana katika huduma yetu,” tamko hilo limeeleza.
Mamlaka mpya ya Baraza Kuu linalosimamia radio and televisheni (RTÜK), ambaye ni mdhibiti wa serikali kwa vyombo vya habari, lilichapishwa wiki hii katika gazette rasmi la serikali ya Uturuki.
Pamoja na mambo mengine, sheria hizo zitalazimisha vyombo hivyo vya habari kuwa na leseni na kulipa ada, na kuruhusu Baraza Kuu (RTÜK) kusimamisha programu mbalimbali na kufuta leseni kama ni vikwazo kwa kutofuata sheria.
Rasimu ya kwanza ya sheria hizo ilitayarishwa mwaka mmoja uliopita, kwa mujibu wa Yaman Akdeniz, mhadhiri anayefundisha sheria katika chuo kikuu cha Istanbul Bilgi ambaye ni mtaalamu wa udhibiti wa mitandao.
Hatua hiyo kuna uwezekano ikawa na athari pana zaidi, amesema, kwa sababu, mtu yeyote anaweza kurusha maudhui kupitia mtandao wa intaneti siku hizi. Kati ya watu 5 wawili nchini Uturuki wanasema wanapata habari zao kupitia mitandao.
Ukitafakari rikodi ya siku za nyuma ya nchi hiyo ya kuzuia au kuwaadhibu waandishi na wapinzani kutumia mitandao, sheria hizo mpya siyo mamlaka ya kutoa leseni, ni mamlaka ya kudhibiti makundi hayo,” amesema mhadhiri huyo.
“Hili ndilo linalotokea Uturuki. Tunazungumzia nchi ambayo inazuia kuingia katika safu ya mtandao wa Wikipedia kwa zaidi ya miaka miwili,” amesema.