UN yasema haina ushahidi walinda amani wake walifyatua risasi kwa raia

Waandamanaji wakipambana na polisi wakati wakiandamana kupiga uwepo wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa MONUSCO katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , huko Sake, takriban kilomita 24 magharibi ya Goma, July 27, 2022.

Waandamanaji wakipambana na polisi wakati wakiandamana kupiga uwepo wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa MONUSCO katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , huko Sake, takriban kilomita 24 magharibi ya Goma, July 27, 2022.

Umoja wa Mataifa umesema hauna ushahidi hadi sasa kwamba walinda amani wake walifyatua risasi kwa raia katika siku tatu za maandamano ya kupinga vikosi vyake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Watu 19 mpaka sasa wamethibitishwa kufariki kutokana na ghasia zilizozuka kwenye miji mitatu inayolenga kambi za UN.

Maafisa watatu wa UN ni miongoni mwa watu waliokufa. Maandamano yalizuka mashariki mwa DRC Jumatatu watu wakiushutumu umoja huo kushindwa kudhibiti ghasia zinazosababishwa na makundi yenye silaha.

Naibu mwakilishi maalumu wa wa UN katika nchi hiyo Kassin Diagne amesema wachunguzi tayari wametumwa kusaidia maafisa wa usalama kutathmini risasi zilizouwa raia kwenye miji ya Butembo na Goma.

Kituo cha walinda amani wa MONUSCO, Goma, DRC chawashwa moto na waandamanaji.

Kituo cha walinda amani wa MONUSCO, Goma, DRC chawashwa moto na waandamanaji.

Bwana Diagne amesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa walinda amani wa UN walitumia nguvu wakati waandamanaji walipovamia kambi zao na kuchoma moto magari , ofisi na kufanya wizi kwenye maduka ya vyakula.

Mjumbe maalum wa UN Diagne anaeleza: "Hatuna ushahidi wowote kwamba wanajeshi wa MONUSCO waliwafyatulia risasi raia. Lakini tunataka kuhakikisha kwamba tunafanya uchunguzi na serikali kutambua ni mahali gani hasa risasi zilitokea.”

Waandamanaji wameshutumu vikosi vya usalama vya Congo kwa mauaji hayo. Hii inakuja wakati ambapo idadi ya vifo inaongezeka baada ya waandamanaji wanne kupigwa na shoti ya umeme siku ya Jumatano katika mji wa Uvira wakati wanajeshi walipofyatua risasi zilizogonga nyaya za umeme zilizowaangukia watu.

Tume hiyo ya DRC ni ya pili kwa ukubwa ya jeshi la walinda amani wa UN duniani, lakini katika miaka ya karibuni walianza kujiondoa na kupunguza vikosi vyao katika maeneo ya nchi.

Farhan Haq, UN deputy spokesperson

Naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Farhan Haq anaeleza: Tuna taarifa kutoka jamhuri ya kidemokrasi ya congo ambako ghasia dhidi ya walinda amani wetu zinaendelea . katika kambi ya MONUSCO , Butembo leo, wavamizi wamepora silaha kutoka kwa polisi wa DRC na kuwafyatulia kwa wanajeshi wetu waliokuwa na sare . inasikitisha , mlinda amani mmoja na afisa wa polisi wa UN wameuwawa na mwingine amejeruhiwa . Tunapaza sauti yetu kwa kaimu mkuu wa monusco Khassim Diagne kulaani mauaji ya wenzetu na kueleza huzuni yetu kubwa kwa familia zao na wenzao.

Wakati huohuo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken anatarajiwa kuzitembelea DRC na Rwanda mwezi ujao kujaribu kupunguza mivutano iliyopo baina ya nchi hizo mbili.

Miongoni mwa agenda ni kuhusu uasi wa kundi la M23, Uchaguzi mkuu na mikataba ya madini.