Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 15:59

Burundi yashutumiwa kupeleka vikosi vyake DRC kupambana na uasi


Picha ya Maktaba ikionyesha vikosi vua Burundi.
Picha ya Maktaba ikionyesha vikosi vua Burundi.

Kundi moja la haki za binadamu nchini Burundi limesema Burundi kwa siri imepeleka mamia ya vikosi na wanachama wa kundi la vijana kwenda nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, operesheni yake kubwa inafahamika kama RED-Tabara, limesema kundi la Burundi Human Rights Initiatives, ikigusia kundi la uasi ambalo bado linafanya shughuli zake na kuchukuliwa kama la kigaidi na serikali ya Burundi.

Mpaka sasa Burundi imekuwa ikikana kufanya oparesheni za siri, ikisisitiza kuhusika na oparesheni za kijeshi za pamoja chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika ama Umoja wa Mataifa.

Burundi ni sehemu ya kikosi cha kikanda kilichokubaliwa cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kukabiliana na makundi ya uasi yanayo sumbua mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

XS
SM
MD
LG