Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:48

Makundi ya kutetea haki za binadamu yaiomba serikali ya DRC kumuachia huru mwandishi wa habari


Nembo ya shirika la wanahabari wasiokuwa na mipaka, Reporters without Borders
Nembo ya shirika la wanahabari wasiokuwa na mipaka, Reporters without Borders

Darzeni ya makundi ya kutetea haki za binadamu yameiomba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kumuachia huru mwanahabari wa DRC aliyekamatwa wiki iliyopita, baada ya maafisa wa ujasusi kumuachilia huru mwanahabari raia wa Marekani aliyekuwa naye.

Tarehe 13 Julai, idara ya ujasusi ya DRC ilimkamata Joseph Kazadi na mwanahabari mmarekani Stavros Nicolas Niarchos katika mji wa kusini mashariki wa Lubumbashi katika mkoa wa Katanga.

Maafisa waliwashikilia wanaume hao wawili katika mji mkuu Kinshasa, afisa mwandamizi wa serikali aliiambia AFP hapo awali, akieleza kuwa wanahabari hao wanadaiwa kufanya mawasiliano yasiyoruhusiwa na makundi yenye silaha.

Niarchos, mwenye umri wa miaka 33, mwanahabari wa kujitegemea anayeripotia majarida ya Marekani The Nation na The New Yorker, aliachiwa huru Jumanne na kuondoka nchini DRC.

Lakini Kazadi ambaye anaripotia gazeti la Lubumbashi na ambaye alikuwa anamsaidia Niarchos kama mfanya kibarua, yeye bado anazuiliwa.

Jana Alhamisi, tawi la Katanga la chama cha vyombo vya habari vya DRC UNPC, limeomba Kazadi aachiwe huru bila masharti yoyote.

Mkuu wa ofisi ya shirika la wanahabari wasiokuwa na mipaka Reporters without Borders kanda ya Afrika, Arnaud Froger, naye ametoa wito wa kuachiliwa huru mara moja mwanahabari huyo.

XS
SM
MD
LG