Kundi hilo limedai kuhusika kupitia taarifa kwenye mtandao wa Telegram bila kutoa maelezo zidi.
Siku ya Ijumaa, mashahidi wawili walisema washambuliaji waliwaua zaidi ya dazeni moja ya watu katika zahanati moja, na kusema uvamizi huo ulitekelezwa na wapiganaji wa Kiislamu wanaoshirikiana na Islamic State.
Kundi hilo lilishambulia kliniki inayoendeshwa na kanisa katika majira ya saa nne usiku wa Alhamisi.
Msemaji wa jeshi Alinukiwa akisema kwamba washambuliaji hao wanatoka katika kundi ambalo linashirikiana na kundi la ADF na kwamba walikuwa wabnatumia mbinu zinanzowiana na zile zinazotumiwa na kundi hilo.
Jeshi liliwaua wapiganaji hao watatu na kumkamata mmjoja baada ya kujibu shambulizi hilo katika mji wa Lume, alisema msemaji wa jeshi Antony Mualushay.