Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 10:34

Mapigano makali yanaendelea kati ya wanajeshi wa DRC na waasi wa M23 licha ya makubaliano ya Angola


Wanajeshi wa DRC katibu na mlima Kibumba unaoshikiliwa na waasi wa M23, kilomita 25km kutoka mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Oct. 27, 2013. PICHA: AP
Wanajeshi wa DRC katibu na mlima Kibumba unaoshikiliwa na waasi wa M23, kilomita 25km kutoka mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Oct. 27, 2013. PICHA: AP

Mapigano makali yametokea mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa kundi la M23, saa chache baada ya rais wa Congo Felix Tshisekedi kukubaliana na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame kupunguza uhasama kuhusiana na mapigano hayo.

Kundi la M23, ambalo serikali ya Jamhuri ya kidemkrasia ya Congo inadai kwamba linasaidiwa na serikali ya Rwanda, lilianzisha mapigano makali mashariki mwa Congo mnamo mwezi March, na kudhibithi mpaka muhimu wa Bunagana na miji mingine miwili licha ya kuwepo juhudi za kijeshi kukabiliana na kundi hilo.

Rwanda imekuwa ikikanusha madai ya kuunga mkono kundi hilo, na badala yake kudai kwamba Congo inaunga mkono kundi la waasi la FDLR lenye nia ya kupindua utawala wa rais Paul Kagame.

Makubaliano ya kusitisha uhasama

Rais wa Rwanda Paul Kagame, na mwenzake wa Congo Felix Tshisekedi, walikutana mjini Angola jana jumatano na wakakubaliana kupunguza uhasama kati yao, Pamoja na kuhakikisha kwamba kundi la M23 linaondoka nchini Congo.

Msemaji wa kundi la M23 Mj. Willy Ngoma amesema kwamba “makubaliano ya Angola ni ya kupotosha na hayana maana yoyote. M23 pekee ndio wanaweza kusaini makubaliano ya kusitisha vita, na makubalinao hayo ni kati yetu na serikali ya Congo.”

Mapigano ya leo yameripotiwa katika sehemu za Kanyabusoro na Kazuba, Rutshuru.

Wakaazi wamekimbia makwao.

Kundi la M23 limedai kwamba limechokozwa

Msemaji wa M23 amesema kwamba mapigano kati yao na wanajeshi wa serikali ya Congo yameanza baada ya wanajeshi wa serikali kushambulia ngome zao katika sehemu ya Kanyabusoro.

Serikali ya Congo haijatoa taarifa kufikia wakati tunaandaa ripoti hii. Juhudi za kumfikia msemaji wa serikali hiyo Sylvain Ekenge hazijafanikiwa.

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imekubali pendekezo la kutuma kikosi cha jeshi la Afrika mashariki kupambana na makundi ya waasi nchini DRC.

DRC imesema kwamba haitaki wanajeshi wa Rwanda kuwa sehemu ya kikosi hicho na rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kwamba “hajamshinkiza mtu yeyote kwamba ni lazima jeshi la Rwanda liwe sehemu ya kikosi hicho.”

XS
SM
MD
LG