Kundi la watu limefanya mauaji ya wagonjwa tisa katika shambulio ndani ya kliniki mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasi ya kongo usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi ya Ijumaa, inalaumu wanamgambo wenye masimamo mkali.
Wanamgambo hao wanaminika na jeshi kuwa ni ADF, kundi kutoka Uganda ambalo limekuwa likifanya harakati zake katika misitu ya Congo kwa miongo kadhaa.
Kundi hili la watu lilishambulia kliniki inayoendeshwa na kanisa katika majira ya saa nne usiku wa Alhamisi kwa mujibu wa mashuhuda wawili, shirika la habari la Reuters linaripoti.
Msemaji wa jeshi amesema washambuliaji hao wanatoka katika kundi ambalo linashirikiana na kundi la ADF na kutumia mtindo wa aina moja.
Jeshi limewauwa wapiganaji hao watatu na kumkamata mmjoja baada ya kujibu shambulizi hilo katika mji wa Lume Kivu Kaskazini, alisema msemaji wa jeshi Antony Mualushay.