Sudan imeanzisha uchunguzi juu ya uhalifu uliofanyika katika mkoa wa Darfur chini ya utawala wa rais wa zamani Omar al Bashir mwendesha mashitaka wa serikali ameeleza.
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka Tagelsir al –Heber kesi hiyo inaweza kusikilizwa nje ya nchi.
Miaka 10 iliyopita Mahaklama ya Kimataifa ya Uhalifu, The Hague, ICC, ilitoa hati ya kukamatwa al –Bashir kwa makosa ya mauaji ya halaiki, makosa ya kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Mapigano kati ya waasi na wanamgambo wanounga mkono serikali yaliana tangu mwaka 2003. Umoja wa mataifa unaeleza watu laki 3 walipoteza maisha.
Omar al-Bashir, alipinduliwa na jeshi mnamo mwezi Aprili 2019 baada ya miezi kadhaa ya maandamano yaliyopelekea kupinduliwa na jeshi la nchi hiyo.