Marekani
Marekani bado iko mbele kuliko mataifa mengine kwa idadi kubwa ya maambukizi ambapo idadi imeongezeka kufikia 640,041 kufikia sasa, vifo vilikuwa 31,002, huku wagonjwa 48,000 wakithibitishwa kupona.
Afrika Mashariki
Tanzania
Katika Kanda ya Afrika Mashariki na maziwa makuu, Tanzania kwa mara ya kwanza Jumatano imeripoti idadi kubwa ya maambukizi. Watu 29 walikutwa na ugonjwa wa corona baada ya kufanyiwa vipimo na hivyo kufanya idadi ya jumla kufikia 88, imesema ripoti ya wizara ya afya ya nchi hiyo. Watu 4 wamefariki, 11 walipona.
Rwanda
Nchini Rwanda idadi ya maambukizi hadi jana ilikua 136 baada ya visa vipya 2 kuripotiwa. Wagonjwa 54 walipona. Lakini kituo cha taifa kinachopima magonjwa ya kuambukiza kimesema, wagonjwa wote waliopona na kurudi nyumbani lazima wafanyiwe vipimo vingine vya haraka ili kuhakikisha kwamba afya yao ni salama.
DRC
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inaendelea kuongoza kwa idadi kubwa ya maambukizi ambapo hadi jana ilifikia 267 baada ya visa vipya 13 kuripotiwa. Watu 22 wamefariki kutokana na corona, 23 walipona.
Uganda
Uganda maambukizi yaliokwisha thibitishwa hadi sasa ni 55. Huko Kenya idadi ya maambukizi ilifikia 225 jana baada ya visa vipya 9 kuripotiwa. Tayari watu 10 wamefariki kutokana na ugonjwa huo, 53 walipona, imesema ripoti ya wizara ya afya ya nchi hiyo.
Bara la Ulaya
Huko bara la ulaya, ubelgiji inaonekana kusumbuliwa zaidi kuliko nchi zingine za bara hilo. Taifa hilo limeripoti maambukizi mapya elfu 1,236 pamoja na vifo 417 katika saa 24 zilizopita.
Spain ambayo ilikuwa imepata afweni siku kadhaa zilizopita imeripoti maambukizi mapya elfu 2,157 na vifo 318 mnamo saa 24 zilizopita.
Italy, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Uholanzi hazijaripoti maambukizi mapya kwa siku ya pili mfululizo.
Sweden haikuripoti kisa kipya, Norway imeripoti kisa kimoja katika saa 24 zilizopita.
Russia
Russia imeripoti maambukizi mapya elfu 3 na 448 pamoja na vifo 34 katika saa 24 zilizopita.
China
China imeripoti visa vipya 46 tangu jana, Korea Kusini imeripoti maambukizi mapya 22, Japan haikuripoti kisa kipya tangu jana.
Iran
Iran pia ambayo ilikabiliwa na wimbi la maambukizi siku za nyuma haikuripoti maambukizi mapya.
Amerika Kusini
Katika kanda ya Amerika kusini, Mexico imeripoti maambukizi mapya 448 na vifo 43 katika saa 24 ziliz