Kiongozi wa chama cha Yesh Atid, Yair Lapid amesema Jumatano dakika chache kabla ya muda wa mwisho wa kufikia makubaliano kukamilika amepata uungwaji mkono.
Muda huo ulikuwa usiku wa manane majira ya Israel akieleza alipata uungwaji mkono wa vyama vyenye wabunge wengi kwenye bunge la Knesset.
Lapid aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook akiahidi kwamba serikali itakayoundwa itawatumikia wananchi wote wa Israeli.
Naftali Bennett ambaye anaongoza chama cha mrengo mkali wa kihafidhina, Yamina party, alitangaza Jumapili kuunga mkono muungano wa Lapid.
Kulingana na makubaliano kati ya Lapid na Bennet, Bennet atahudumu kama Waziri Mkuu kwa kipindi cha miaka miwili, baadaye amuachie nafasi hiyo Lapid.