Waziri Mkuu Mohamed Roble alimfuta kazi Waziri huyo Jumatano lakini Rais Mohamed Abdulahi “Farmajo” aliipinga hatua hiyo.
Roble aliziba nafasi ya Waziri wa Usalama Hassan Hundubey Jimale kwa kumteuwa Abdulahi Mohamed Nur.
Lakini Alhamisi Rais Farmajo alisema hatua hiyo haikufuata utaratibu wa Katiba.
Hii ni mara ya pili rais na waziri mkuu wanapingana katika uteuzi wa maofisa.
Hii ni baada ya mkuu wa upelelezi kukaidi amri ya kutoa ripoti ya kina ya kupotea kwa afisa wa ujasusi ndani ya saa 48.
Viongozi hao wawili katika siku zilizopita walitofautiana hadharani juu ya sera.
Rais Farmajo amepiga marufuku mikataba na mashirika ya kigeni hadi baada ya uchaguzi lakini waziri mkuu aliendelea kutia saini makubaliano katika ziara yake ya Kenya mwezi uliopita.