Familia hiyo ilitangaza kupitia ujumbe akaunti yake Jumapili kuwa msanii huyo mwenye umri wa miaka 73, alikuwa hapo awaliamelazwa hospitali Alhamisi na kuwa amewekewa kifaa cha kupumulia Jumamosi Usiku. Ujumbe huo kupitia akaunti ya Twitter ulisema “hali yake ni mbaya.”
Mke wake Prine na meneja Fiona Whelan Prine walitangaza mapema mwezi huu kuwa alikuwa amegunduliwa kuwa na virusi, na mt una mkewe walikuwa wamejizuia kutoka nyumbani na pia kujitenga wao wawili.
Prine amekuwa ni mwimbaji mwenye ushawishi mkubwa na mtunzi wa nyimbo aina za kiasili (country/ folk) kwa takriban miaka 50. Nyimbo zake zimeimbwa na wasanii kama vile Bonnie Rait, Johnny Cash na Bette Midler. Hivi karibuni alikuwa ametambulishwa katika ukumbi wa umaarufu wa waimbaji na watunzi wa nyimbo wa Marekani.
Prine aliwahi kuugua saratani mara mbili na iliathiri sauti yake. Aliweza kupona kwa kiwango kikubwa na kurikodi nyimbo iliyotoka mwaka 2019 na alikuwa na mpango wa kufanya mizunguko mwaka huu kabla ya mlipuko wa virusi vya corona.