Wameeleza hatari imekuwa ikiongezeka na kudumaza mazungumzo juu ya kufufua tena makubaliano ya nyuklia ya Iran.
Wanadiplomasia watatu ambao hufuatilia kwa karibu idara ya nishati ya Atomic (IAEA), walisema safari ya Grossi kabla ya mkutano wa wiki ijayo, wa bodi ya magavana wa mataifa 35 ya IAEA, ilithibitishwa.
Wawili walisema Grossi alitakiwa kuwasili Tehran, mapema Jumapili na kukutana na mkuu mpya wa idara ya nishati ya Atomic ya Iran, Mohammad Eslami.
IAEA ilizijulisha nchi wanachama wiki hii, kwamba hakuna maendeleo juu ya maswala mawili makuu, moja likiwa kuelezea kuhusu uranium iliyogundulika katika maeneo kadhaa ya zamani.
Jambo la pili ni suala la maeneo ambayo hayajatangazwa na kupatiwa fursa ya haraka kufuatilia baadhi ya vifaa, ili idara iweze kuendelea kufuatilia sehemu za mpango wa nyuklia wa Iran, kama ilivyotolewa kwenye makubaliano ya mwaka 2015.