Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:10

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.9 latokea Iran


Tetemeko limetokea katika jimbo la kusini la Iran la Bushehr, ambako kituo cha nishati cha nyuklia kipo.
Tetemeko limetokea katika jimbo la kusini la Iran la Bushehr, ambako kituo cha nishati cha nyuklia kipo.

Tetemeko la ardhi lenye nguvu za 5.9 kwenye kipimo cha Richter limetokea Jumapili katika jimbo la kusini la Iran la Bushehr, ambako kituo cha nishati cha nyuklia kipo, lakini lakini televisheni ya nchi hiyo inasema hapakuwa na repoti za hapo hapo juu ya uharibifu mkubwa wowote. 

Afisa wa serikali ya Iran ameiambia Reuters kuwa hakuna repoti ya uharibifu kutoka katika jengo la nyuklia la Bushehr liliyopo katika pwani ya Ghuba ya Iran.

Kitovu cha tetemeko hilo kinapatikana karibu kilomita 100 (maili 60) kutoka kiwanda hicho cha nyuklia na kwa kiasi fulani lilikuwa na kina kidogo chini cha kilomita 10, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran – ambacho kingeweza kuzidisha mtikisiko.

Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti mitetemeko midogo 16 baada ya tetemeko kubwa na walichapisha picha zilizokuwa zinaonyesha kuporomoko kwa kuta za matofali katika baadhi za nyumba katika vijiji vya karibu.

Saeed Kashmiri, mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Bushehr amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba watu watano walijeruhiwa huko Gonaveh na wamepelekwa hospitali.

Jamhuri ya Kiislam ya Iran inapatikana katika eneo lenye ufa chungu nzima chii ya ardhi na hivyo kua ni moja ya nchi zilizohatarini kwa mitetemeko ya ardhi duniani. Mwaka 2003 tetemeko lenye nguvu za 6.6 kwenye kip[imo cha Richter lilitikisa jimbo la Kerman na kusababisha vifo vya watu 31,000 na kuangamiza kabisa mji wa kale wa Bam.

XS
SM
MD
LG