Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:19

Marekani yaitaka Iran kufanya maamuzi ya haraka kuhusu ya mazungumzo ya nyuklia


Waziri wa mabo ya nje wa Marekani Antony Blinken azungumza na waandishi wa habari mjini Kuwait City, Kuwait, July 29, 2021.
Waziri wa mabo ya nje wa Marekani Antony Blinken azungumza na waandishi wa habari mjini Kuwait City, Kuwait, July 29, 2021.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, alisema Alhamisi kwamba mazungumzo ya kufufua makubaliano ya nyuklia ya 2015 na Iran, "hayawezi kuendelea bila kikomo," akiashiria kwamba ni juu ya Tehran kusonga mbelena kufanya maamuzi ya haraka juu ya suala hilo.

Blinken alizungumza akiwa nchini Kuwait wakati wa kikao na waandishi wa habari, pamoja na mwenzake wa Kuwait, Sheikh Ahmed Nasser Al Mohammed Al Sabah.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Marekani amesema utawala wa Biden uko tayari kuendelea na mazungumzo, lakini ni jukumu la Iran kufanya uamuzi.

Pande hizo mbili zimefanya mazungumzo kadhaa ya moja kwa moja mjini Vienna, Austria, tangu Rais wa Joe Biden aingie madarakani mwezi Januari mwaka huu. Majadiliano yamekuwa ni kuhusu Iran kuheshimu mkataba wa kimataifa ambao ulinuia kudhibiti programu yake ya nyuklia, ili iondolewe vikwazo.

Marekani ilijiondoa kwenye makubaliano ambayo yanajulikana rasmi kama Mpango wa Utekelezaji wa Pamoja, au JCPOA, mnamo mwaka wa 2018, na tangu wakati huo, Iran imechukua hatua kadhaa kinyume na ahadi zake, pamoja na kuimarisha uranium kwa kiwango cha juu, tofauti na masharti ya makubalianao hayo.

XS
SM
MD
LG