Miongoni mwa ajenda zitakazo zungumziwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa, uchumi, afya ya dunia na masuala ya Ugavi.
Harris aliwasili Paris Jumanne kwa ajili ya ziara ya siku nne yenye lengo la kuondoa mivutano kuhusu makubaliano ya manowari ya nyuklia.
Uhusiano wa Washington na Paris ulishuka kihistoria mwaka huu baada ya makubaliano ya manowari kati ya Marekani na Uingereza na Australia na kuvuruga makubaliano ya Ufaransa na wa β Australia.
Kabla ya kukutana na Macron, Harris na mume wake Doug Emhoff walitembelea taasisi mashuhuri ya Pasteau mjini Paris Jumanne na kukutana na wanasayansi wa Marekani na Ufaransa wanaoshughulikia COVID -19 na kujiandaa na janga ulimwenguni.
Maafisa wanasema ziara hiyo inasisitiza mabadilishano ya kisayansi ya muda mrefu kati ya Marekani na Ufaransa na azimio la kukabaliana na changamoto za ulimwengu hasa katika kumaliza janga hili kimataifa.
Wameongeza kuwa : βSio tu ishara ya hali ya sasa ya uhusiano na kujitolea kwetu kwa siku zijazo lakini pia ni taarifa ya kipekee kuhusu historia ya uhusiano kati ya Ufaransa na Marekani kuhusu masuala mengi, lakini hasa juu ya utafiti wa kisayansi.
Baadhi ya uvumbuzi muhimu katika sayansi kwa suala lolote kuanzia ugonjwa wa kichaa cha mbwa hadi UKIMWI , saratani ya matiti , mRNA na yale tunayofanya kwa chanjo na magonjwa ya milipuko yametokea hapa kwa ushirikiano na wanasayansi wa Ufaransa, wanasayansi wa Marekani, wanasayansi wa ulimwenguni kote.β