Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:35

Waziri Blinken apiga hatua katika kuimarisha uhusiano bora na Ufaransa


Antony Blinken alipokutana na Katibu Mkuu wa OECD Mathias Cormann wa Ufaransa, makao makuu ya OECD Ufaransa, Juni 25, 2021.Andrew Harnik/Pool via REUTERS
Antony Blinken alipokutana na Katibu Mkuu wa OECD Mathias Cormann wa Ufaransa, makao makuu ya OECD Ufaransa, Juni 25, 2021.Andrew Harnik/Pool via REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken Jumatano amekamilisha ziara yake mjini Paris kwa kufanya mazungumzo na mawaziri wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo baada ya kusukuma kurejesha uhusiano bora wa Marekani na Ufaransa.

Blinken ameiambia jumuiya ya OECD mjini Paris Jumanne kwamba janga la virusi vya corona na mabadiliko ya hali ya hewa yamezidisha ukosefu wa usawa kati na ndani ya mataifa, na kuwa lazima hatua zichukuliwe ili kubadili mwenendo huo.

"Data ziko wazi. vyote janga na mabadiliko yahali ya hewa viemathiri sana watu wenye hali ngumu katika jamii zetu. Tunaliona hili Marekani katika jumuiya za walio wachache zimeathiriwa sana idadi kubwa ya vifo kutokana na COVID-19 pamoja na athari kubwa za mabadiliko ya hali ya hewa. Sote tunabeba jukumu Fulani katika hili.

Kwa miongo kadhaa, nchi wanachama wetu wamepima mafanikio ya kiuchumi haswa kwa ukuaji wa pato la taifa la ndani - GDP na masoko ya hisa ambavyo havionyeshi ukweli wa mabilioni ya familia za kazi badala yake ukuaji wetu ambao hauwajawahi kutokea mara kwa mara umekuwa na ukuaji usio wa uwiano," ameeleza Waziri Blinken.

Sehemu ya kwanza ya mkutano wake wa Paris ililenga katika kurekebisha uhusiano uliokuwa na mvutano na mshirika wake ufaransa kufuatia mzozo kuhusu ushirikiano wa usalama baina ya marekani, uingereza na Australia.

XS
SM
MD
LG