Viongozi hao wawili watalenga kurejesha uaminifu kati ya nchi hizo, imesema taarifa iliyotolewa na ofisi ya Le Drian.
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Ufaransa ulishuka chini sana mwezi uliopita, baada ya Australia kufuta makubaliano ya awali ya ujenzi wa meli aina ya submarine yenye thamani ya dola bilioni 40 kati yake na Ufaransa na badala yake ikaingia mkataba wa meli aina ya submarine 8 zinazoendeshwa na nishati ya nyuklia kati yake na teknolojia ya Marekani na Uingereza.
Katika hali ya kulipiza kisasi, Ufaransa ilimuondoa balozi wake kwa muda mfupi kutoka Marekani, japokuwa tangu wakati huo balozi huyo amerejea Washington.
Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron tayari wamefanya mazungumzo baada ya mgogoro huo wa makubaliano ya meli ya submarine kutokea, akiahidi kuanza “mashauriano ya kina” katika ushirikiano wa pande mbili.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters