Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 10:40

Marekani kuimarisha tena uhusiano wake na Ufaransa


Rais wa Marekani Joe Biden,(kushoto) ,na mwenzake wa Ufaransa Eammanuel Macron kwenye picha ya awali .
Rais wa Marekani Joe Biden,(kushoto) ,na mwenzake wa Ufaransa Eammanuel Macron kwenye picha ya awali .

Marais wa Marekani na Ufaransa Jumatano wamekubaliana kuboresha uhusiano kati ya nchi zao kuendelea mbele.

Ufaransa ikikubali kwa upande wake imekubali kumrudisha balozi wake mjini Washington wakati White House ikisema ilifanya makosa kwa kuingia mkataba na Australia ambayo ilinunua teklonojia ya Marekani ya manowari za kijeshi badala ya ile ya Ufaransa, bila kushauriana na Paris.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya rais Joe Biden na rais Emmanuel Macron kuzungumza kwa njia ya simu, viongozi hao wawili wamekubaliana kuanzisha mashauriano ya kina ili kujenga tena imani, na kukutana barani Ulaya mwishoni mwa mwezi Oktoba. Wamesema Washington imeahidi kuunga mkono operesheni za kupambana na ugaidi katika ukanda wa Sahel zinazoendeshwa na nchi za ulaya.

Mazungumzo ya simu ambayo yaliombwa na Washington, yalikuwa jaribio la kumaliza mvutano baada ya Ufaransa kuishtumu Marekani kwa ‘kuisaliti’ Ufaransa, wakati Australia iliweka kando kandarasi ya dola billioni 40 kwa ununuzi wa manowari za kawaida za Ufaransa, na kuchagua manowari zinazotumia nyuklia kujengwa na teknolojia ya Marekani na Uingereza badala ya ile ya Ufaransa.

Ufaransa ilikasirika kutokana na makubaliano hayo ya ushirikiano wa kiusalama kati ya Marekani, Uingereza na Australia, na kuwaita nyumbani mabalozi wake kutoka Washington na Canberra.

XS
SM
MD
LG