Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:15

Mapinduzi ya kijeshi Sudan yaweka njia panda msamaha wa deni la Ufaransa


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alipozungumza katika mkutano wa New Africa-France 2021 humo Montpellier, kusini mwa Ufaransa Oktoba 8, 2021.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alipozungumza katika mkutano wa New Africa-France 2021 humo Montpellier, kusini mwa Ufaransa Oktoba 8, 2021.

Mapinduzi nchini Sudan yanatia shaka mchakato ambao ungeifanya Ufaransa kufuta deni la dola bilioni 5 iliyokuwa inaidai nchi hiyo, wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilisema

Mapinduzi nchini Sudan yanatia shaka mchakato ambao ungeifanya Ufaransa kufuta deni la dola bilioni 5 iliyokuwa inaidai nchi hiyo, wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilisema Ijumaa, ikiwa ni nguvu ya hivi karibuni kuwashinikiza viongozi wa kijeshi walionyakua mamlaka.

Ufaransa, mkopeshaji mkuu wa pili wa Sudan, imekuwa ikichukua nafasi ya juu katika kuunga mkono mamlaka ya muda baada ya Rais wa zamani Omar al-Bashir kuondolewa madarakani mwaka 2019, lakini mabadiliko ya kiraia yalikwama mwezi Oktoba wakati jeshi lilipochukua udhibiti.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kila siku Ijumaa, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Anne-Claire Legendre alisema Paris imekuwa mshirika asieyumba wa Sudan na kwamba mpango wa jumla wa kufuta madeni kama sehemu ya mpango wa Nchi Maskini zenye madeni makubwa (HIPC) ulikubaliwa katika mkutano huko Paris mwezi Mei.

Makubaliano ya Klabu ya Paris yalifikiwa Julai 15, kila mdai sasa alipaswa kutia saini makubaliano ya pande mbili na Sudan, Legendre aliwaambia waandishi wa habari,wakati akijibu swali kama Paris inaangalia upya ahadi yake ya kufuta deni.

Ni wazi kwamba mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba 25 yanatia shaka mchakato huu aliongeza.

Sudan inadaiwa karibu dola bilioni 60, asilimia 40 kati yake au dola bilioni 23.5 zinashikiliwa na Klabu ya Paris.

XS
SM
MD
LG