Israeli yakamilisha matayarisho ya uchaguzi wa Jumanne

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Maafisa wa uchaguzi wa Israel wajitayarisha kwa uchaguzi muhimu wa nne wa bunge katika kipindi cha miaka minne Jumanne.

Kesho itakuwa ni sku ya mapumziko pale wapiga kura mlioni 6.5 walojiandikisha watakapo kwenda kupiga kura kwenye vituo elfu 12 127, vilivyowekwa ndani ya shule za nchi hiyo.

Kwa mara nyingine Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu aliyeko madarakani kwa miaka 12 anagobania tena nafasi yake akiwa anakabliwa na mashtaka ya uhalifu.

Netanyahu, ambae ni Waziri Mkuu wa kwanza kufunguliwa mashtaka ya uhalifu akiwa madarakani anatarajiwa kushinda, lakini hatoweza kupata viti 61 vinavyohitajika kuunda serikali kulingana na uchunguzi wa maoni. Uchaguzi huu unakabiliwa na ushindani mkubwa kutokana na kujitokeza vyama vipya vya mrengo wa kulia.

Hivyo kuwepo uwezekano wa mvutano wa kutoweza kuunda serikali baada ya uchaguzi wa tano mfululizo, ikiwa ni historia katika nchi hiyo.

Nchini Israel wapiga kura huchagua vyama na wala si wagombea mmoja mmoja na chama cha Waziri Mkuu cha Likud cha tazamiwa kupata ushindi.