Wanachi wa Israeli huenda wakalazimika kupiga kura kwa mara ya nne katika kipindi cha mwaka mmoja iwapo kiongozi wa upinzani Benny Gantz atashindwa kuunda serikali ya mseto ifikapo usiku Jumatatu.
Jumapili, Rais Reuven Rivlin alikataa ombi la ,Gantz, kiongozi huyo wa chama cha white and Blue kuongezewa muda wa wiki mbili kuweza kumaliza mazungumzo ya kunda serikali ya mseto ya dharura na chama cha Likud cha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Rais Rivlin amesema kutokana na hali ya dharura ya kupambana na COVID 19 hataongeza muda.
Wachambuzi wanasema hali hiyo imempa nguvu Netanyahu anaye kabiliwa na mashtaka ya tuhuma za ulaji rushwa.
Iwapo pande hizo mbili zitshindwa kufikia makubaliano leo bunge litakuwa na jukumu la siku 21 kumteua mtu mwengine kuunda serkali na ikishindikana Waisrael watalazimika kupiga kura kwa mara ya nne.